Matthew 4:12-17

12 aIsa aliposikia kwamba Yahya Mbatizaji alikuwa ametiwa gerezani, alirudi Galilaya. 13 bAkaondoka Nasiri akaenda kuishi Kapernaumu, mji ulioko karibu na bahari, katika mipaka ya nchi ya Zabuloni na Naftali, 14 cili kutimiza unabii wa nabii Isaya, kama alivyosema:
15 d“Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali,
kwenye njia ya kuelekea baharini,
ng’ambo ya Yordani,
Galilaya ya watu wa Mataifa:

16 ewatu wale waliokaa gizani
wameona nuru kuu;
nao wale walioishi katika nchi ya uvuli wa mauti,
nuru imewazukia.”

17 fTangu wakati huo, Isa alianza kuhubiri akisema: “Tubuni, kwa maana Ufalme wa Mbinguni umekaribia.”

Isa Awaita Wanafunzi Wake Wa Kwanza

(Marko 1:16-20; Luka 5:1-11)

Copyright information for SwhKC